pmbet

Ukraine yaishambulia Urusi kwa kombora jipya la Flamingo

Eric Buyanza

June 11, 2026
Share :

Ukraine imesema imefanya mashambulizi ndani ya Urusi kwa kutumia kombora lake la kutengenezwa nchini humo aina ya Flamingo, hatua inayodhihirisha kuimarika kwa uwezo wake wa kijeshi zaidi ya miaka minne tangu kuanza kwa vita.
 

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema kombora hilo lililenga kiwanda cha kijeshi katika mji wa Cheboksary, takriban kilomita 1,000 kutoka mpaka wa Ukraine, ambacho hutengeneza vifaa vya droni na makombora kwa ajili ya jeshi la Urusi.

 

Gavana wa eneo hilo la Chuvashia, Oleg Nikolayev, amethibitisha shambulio hilo na kusema mamlaka zinaendelea kutathmini uharibifu na idadi ya walioathirika.

 

Jeshi la Ukraine pia limesema lilishambulia kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la Samara pamoja na meli ya mafuta ya Urusi katika Bahari Nyeusi.

 

Kombora la Flamingo ni miongoni mwa silaha mpya zilizotengenezwa na Ukraine, ingawa matumizi yake bado ni nadra.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet