Ukraine yasema imedungua Droni 59 na Makombora ya Urusi
Eric Buyanza
May 8, 2024
Share :
Jeshi la anga la Ukraine limedungua makombora na kuzuia mashambulizi ya droni zilizorushwa na Urusi usiku kucha na zilizolenga vituo vya nishati vya Ukraine.
Kupitia ukurasa wa Telegram, jeshi hilo limesema kuwa Urusi ilifanya mashambulizi 76 ya anga, kwa kutumia makombora 55 na droni 21 na kwamba mfumo wake wa ulinzi wa anga ulifanikiwa kuzuia makombora 39 na droni 20.
Hata hivyo, mamlaka imeeleza kuwa mashambulizi hayo yamesababisha majeruhi ya watu watatu - wawili karibu na eneo la mji mkuu Kyiv na mwengine mmoja katika mkoa wa kati ya Kirovograd.
Hivi karibuni, Urusi imezidisha mashambulizi dhidi ya vituo vya nishati vya Ukraine na kusababisha kukatika kwa umeme na kuathiri mgao wa nishati nchini Ukraine.