pmbet

Ukraine yatuma droni 24 kuushambulia mkoa wa Kursk nchini Urusi

Eric Buyanza

July 29, 2024
Share :

Ukraine imerusha zaidi ya Droni 24 kuupiga mkoa wa Kursk nchini Urusi ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kijeshi iliyoanza siku ya Jumamosi usiku ambayo imefanikiwa kuharibu bohari ya mafuta katika mkoa huo. 

Hayo yamethibitishwa na kaimu gavana wa mkoa huo unaopakana na Ukaine, Andrei Smirnov ambaye pia alisema Droni 13 za Ukraine zilidunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi ikiwa ni siku moja tu tangu droni nyingine 19 za Ukraine kuharibiwa zikiwa njiani kuulenga mkoa huo.

Andrei amesema mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mdogo kwenye majengo ya makazi lakini hakutoa ufafanuzi zaidi kuhusu athari zilizotokea.

Katika miezi ya karibuni Ukraine imekuwa ikiilenga miundombinu ya nishati na kijeshi ya Urusi kwa dhamira ya kuvuruga uchumi wa nchi hiyo na uwezo wake wa kuendelea na vita vilivyoanza kwa uvamizi wa jeshi la Urusi mnamo Februari 2022.
DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet