Ukumbi wa harusi ya Davido na Chioma wazua gumzo mitandaoni.
Joyce Shedrack
June 29, 2024
Share :
Siku chache mara baada ya kukamilika kwa sherehe ya harusi ya mkali wa Afrobeat kutoka Nchini Nigeria Davido pamoja na mpenzi wake Chioma iliyofungwa siku ya Jumanne Juni 25,2024 huko Lagos Nchini Nigeria iliyo-trend ndani na nje ya mipaka ya Afrika.
Harusi hiyo imeendelea kubaki kwenye vinywa na midomo ya watu haswa baada ya kusambaa kwa video ikionyesha ukumbi uliotumika kwenye sherehe hiyo na namna ulivyopendezeshwa kwa mapambo ya kuvutia.
Harusi hiyo ilitikisa Afrika nzima kutokana uwepo wa watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali ikiwemo siasa,burudani na michezo wengi waliolikwa kwenye harusi hiyo walikuwa ni watu wenye nguvu kubwa kifedha.
Baada ya harusi hiyo Davido na Mke wake Chioma waliondoka Nigeria kwa ndege yao binafsi kuelekea kwenye mapumziko ya fungate ambayo hayakuwekwa wazi wanaelekea Nchi gani.
Wawili hao walianza mahusiano yao mwaka 2013 na kuchumbiana mwaka 2019 jijini London.