pmbet

Ulaji wa Zabibu za aina hii hutibu tatizo la nguvu za kiume

Eric Buyanza

January 26, 2024
Share :

Tatizo la nguvu za kiume limekuwa janga kubwa kwa dunia ya sasa na hivyo kuwalazimu wasomi kuingia maabara kila leo ili kuona namna ya kupata suluhisho ya jambo hili.

Profesa Aidan Cassidy katika Chuo Kikuu cha Malkia huko Belfast (Ireland ya Kaskazini) amefanya utafiti ikiwa wanaume wanaweza kutumia zabibu nyeusi kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Anasema kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na mtiririko wa damu usiofaa.

'Anthocyanin, flavinoid zinazopatikana katika zabibu nyeusi (ambazo hupatia tunda rangi ya zambarau), huboresha mtiririko wa damu,' anasema.

Hii huifanya mishipa ya damu kunyumbulika na kufunguka.'

Uchunguzi wa kina wa miaka 10 wa wanaume zaidi ya 25,000 uligundua kwamba wale waliokula matunda ya anthocyanin au zabibu nyeusi mara tatu au zaidi kwa wiki walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet