pmbet

Ulevi wamponza Travis Scott ajikuta mikononi mwa Polisi.

Joyce Shedrack

June 20, 2024
Share :

Rapa kutoka Nchini Marekani Travis Scott amekamatwa na polisi  katika mji wa Florida kwa tuhuma za kuanzisha vurugu akiwa amelewa.

Rapa huyo ambaye jina lake kamili ni Jacques Bermon Webster mwenye umri wa miaka 33,  alitiwa mbaroni na polisi katika Miami Beach Marina mapema Alhamisi asubuhi na kufungwa jela ya kaunti hiyo kwa kosa la ulevi na kuanzisha vurugu jambo lilisosababisha watu waliokuwa eneo hilo kuwapigia simu polisi ili wafike.

 

Mashuhuda wa tukio wanasema baada ya polisi kuwasili mwanamuziki huyo aligoma kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi na baadae polisi kumchukua kwa nguvu na kwenda naye kituoni.

 

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku chache kabla hajaanza ziara yake ya barani Ulaya itakayoanzia Netherlands  ijumaa ya wiki ijayo.

 

Hii siyo mara ya kwanza kwa rapa huyo kujikuta mikononi mwa polisi kutokana na matukio anayoyafanya kwani mara kadhaa amejikuta akikabiliwa na makosa mbalimbali.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet