Ulikuwa ni usiku mbaya kwa Simba na Tanzania
Eric Buyanza
April 6, 2024
Share :
Ulikuwa usiku mbaya kwa Tanzania pale klabu ya Simba nayo ilipokwaa kisiki kusonga mbele michuano ya klabu bingwa.
Simba walikubali kichapo cha bao 2-0 mbele ya Al Ahly ya Misri mjini Cairo, hii ni baada ya wiki iliyopita kukubali kichapo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa miamba hao wa misri kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Amr el Solia ndiye aliipatia Al Ahly bao la kwanza mnamo dakika ya 47 na Mahmoud Kahraba aliongeza la pili kupitia mkwaju wa penalti wakati wa dakika za nyongeza.
Al Ahly watacheza na mshindi wa mechi ya leo kati ya wenyeji Petro Luanda ya Angola na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.