Umaarufu hauji kwa kuvaa nguo fupi - Uwoya
Eric Buyanza
September 2, 2025
Share :
Msanii wa Bongo Movie, Irene Uwoya amesema anachoangalia kwenye mavazi yake ni kupendeza na siyo gharama, huku akikemea wasanii wanaovaa nusu uchi.
“Unajua mimi siwezi kukuambia ninavaa nguo za gharama fulani ya juu, hapana, navaa tu ili mradi ikikaa kwenye mwili wangu inanipendeza, si nguo tu hata nywele navaa zozote zile ili mradi nipo smati,” alisema Uwoya.
Alisema, umaarufu ni gharama na hauji kirahisi kama watu wanavyofikiria ama kudhani eti huwezi kuwa nyota bila kuvaa nguo nusu utupu, akidai huvaaji wa hivyo haumpendezi hata Mungu na mashabiki wengi.
"Kuna wakati lazima wasanii hasa chipukizi watambue umaarufu hauji kwa kuvaa nguo fupi au kashfa, Mungu kwanza hapendi kabisa mtu au msanii kuvaa mavazi ya utupu, wafanye kazi ndiyo watafika mbali," alisema Irene.
MWANASPOTI