Umeme hautakatika kwenye Treni ya SGR
Eric Buyanza
February 26, 2024
Share :
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini (TRC), Bw.Masanja Kadogosa amesema Watanzania wasiwe na wasiwasi wa kwamba treni inaweza kuzimika ikiwa njiani kisa umeme, kwa sababu njia ya umeme (Transmission Line), unaotumika katika kuendesha Treni ya Umeme ya Kisasa ya (SGR), inajitegemea.
Bwana Kadogosa amesema ili treni isimame kwa sababu ya umeme, labda kama nchi nzima umeme uwe umekatika jambo ambalo sio rahisi kutokea.