pmbet

Ummy awasilisha Ujumbe wa Rais Samia kwa Marais wa nchi 5

Sisti Herman

July 14, 2024
Share :

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan amefanya ziara kwenye Nchi tano tofauti kuanzia Julai 08,2024 hadi Julai 13,2023 akiwa na ujumbe maalum wa Rais Samia ambao ameukabidhi kwa Marais wa Nchi hizo ambapo kwa kuanzia July 08,2024 aliwasilisha ujumbe maalum wa Rais Dkt Samia kwa Rais wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde.

Waziri Ummy July 10,2024 aliwasilisha pia ujumbe wa Rais Samia kwa Rais wa Guinea, General Mamadi Doumbouya ambao ulipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea Dkt. Morrisanda Kouyate ambapo akikabidhi ujumbe huo Waziri Ummy amesema ili kudhihirisha urafiki wa kidugu kati ya Guinea na Tanzania kuna barabara kubwa katika Jiji la Dar es salaam inayoitwa Toure Road na Hospitali ya Sekou Toure iliyopo Jijini Mwanza ambao ni mji wa pili kwa ukubwa Nchini Tanzania wakati Guinea kuna Chuo Kikuu cha Julius Nyerere University of Kankan (UJNK).

Ummy akiwa anaendelea na uwasilishaji wa ujumbe amefika Mauritania July 11,2024 na kuwasilisha ujumbe wa Rais Samia kwa kwa Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani, ujumbe huo umepokelewa naMohamed Bilal, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritania.

Waziri Ummy July 12, amewasilisha ujumbe wa Rais Samia kwa Adama Barrow, Rais wa Jamhuri ya Gambia Jijini Banjul, ambapo Barrow baada ya kupokea ujumbe huo maalum amesema Gambia na Tanzania zimekuwa zinashirikiana katika nyanja mbalimbali kwa muda mrefu.

Waziri Ummy July 13,2024 amewasilisha ujumbe huo maalum kwa Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu ambapo ujumbe huo wa Rais Samia umepokelewa na Yusuf Maitama Tuggar Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet