pmbet

Umoja wa mataifa wapitisha ramani mpya ya Afrika

Eric Buyanza

September 5, 2026
Share :

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) limepitisha azimio la kihistoria linalolenga kuachana na ramani ya zamani ya dunia na kuanza kutumia ramani mpya inayonyesha ukubwa halisi wa kijiografia wa Bara la Afrika.

 

Azimio hilo linalojulikana kama "Correct the Map" (Rekebisha Ramani), liliwasilishwa rasmi na nchi ya Togo kwa niaba ya Kundi la nchi za Afrika na kuungwa mkono kwa dhati na Umoja wa Afrika (AU). Katika upigaji kura uliokamilika Ijumaa, Septemba 4, 2026, jumla ya mataifa 164 yalipiga kura ya NDIO, nchi sita (6) zikajizuia, huku Marekani ikiwa nchi pekee duniani iliyopiga kura ya HAPANA.

 

Tangu mwaka 1569, dunia imekuwa ikitegemea mfumo wa ramani wa Mercator Projection, uliotengenezwa na mchoraji wa ramani wa Flemish, Gerardus Mercator. Lengo kuu la ramani hiyo lilikuwa kusaidia mabaharia wa Ulaya kuvuka bahari kwa kutumia dira, lakini ilileta upotoshaji mkubwa wa maeneo ya kijiografia kwa kupanua maeneo yaliyo karibu na ncha za dunia na kusinyaisha maeneo yaliyo karibu na Ikweta.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet