Umtiti awavaa wanaoshinda tuzo bila timu zao kuwa na mataji
Sisti Herman
September 14, 2026
Share :

Aliyekuwa beki wa Ufaransa na Barcelona Samuel Umtiti amekosoa mchakato wa upigaji kura wa tuzo ya Ballon dโOr na umuhimu ambao wachezaji huipa tuzo hiyo.
โWanamjumuisha Juliรกn Quiรฑones, lakini alifanya nini kwenye Kombe la Dunia? Mabao manne akiwa na Mexico na kutolewa katika hatua ya 16 bora? Nilipoona hivyo, nilijiuliza kama ilikuwa ni ๐ฏ๐ข๐๐ก๐๐ค๐๐ฌ๐ก๐จ.โ
โKuna upendeleo mkubwa katika soka, ambalo ni mchezo wa timu. Watu wanawaza sana kuhusu ๐ค๐ฎ๐ฌ๐ก๐ข๐ง๐๐ ๐๐๐ฅ๐ฅ๐จ๐ง ๐โ๐๐ซ kuliko mafanikio ya pamoja.โ
โUnaweza kushinda Ligi ya Mabingwa na timu yako lakini ukawaza kuhusu wewe mwenyewe tu. Tuzungumzie takwimu wakati mwingine, kwa sababu hazitoshi. Soka ๐ฌ๐ข ๐ฌ๐ฎ๐ฅ๐๐ฅ๐ ๐ฅ๐ ๐ญ๐๐ค๐ฐ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ฉ๐๐ค๐๐.โ
โTangu enzi za Messi na Ronaldo, hata siifuatilii tena tuzo hiyo. Walikuwa na takwimu za ajabu, na hata kama hawakushinda taji kubwa, haikuwa na maana kubwa kwa sababu msimu wao ulikuwa wa kipekee.โ
โSiku hizi, hakuna mchezaji mmoja mahiri anayewazidi wengine kwa kiasi kikubwa,โ Umtiti aliliambia shirika la RMC Sport.





