pmbet

Umuhimu Himid Mao, Kagoma na Abuya kwenye Rest Defence za timu zao.

Sisti Herman

July 8, 2026
Share :

Utangulizi

Takwimu za Ligi kuu ya NBC zinaonyesha kuwa timu za Simba SC, Yanga SC na Azam FC ndiyo timu 3 za juu zinazoongoza kwa wastani mkubwa wa umiliki mkubwa wa mpira.

 

1. Simba SC – umiliki wa mpira 57.5%

2. Young Africans SC – umiliki wa mpira 55.8%

3. Azam FC –umiliki wa mpira 55.2% 

 

Wastani mkubwa wa umiliki wa mpira umesaidia timu hizo kuwa na muda na nafasi zaidi ya kutengeneza nafasi za kufunga na takwimu zinathibitisha kuwa timu hizo 3 zinaongoza kwa idadi kubwa ya magoli kama ifuatavyo;

 

1. Young Africans SC - magoli 71

2. Simba SC - magoli 54

3. Azam FC - magoli 46

 

Licha ya kuwa umiliki mkubwa wa mpira kuwa na faida ya kutengeneza nafasi nyingi za magoli kwa timu hizo lakini pia umiliki mkubwa wa mpira umezifanya timu hizo kuongoza kufanyiwa mashambulizi ya kujibu (counter attacks).

 

Kwanini timu hizo hufanyiwa Counter Attacks mara nyingi?

Kwasababu ya ubora wa wachezaji wa timu hizo 3, kumiliki mpira, kutengeneza nafasi nyingi na kufunga magoli mengi, timu zingine zinapokutana nazo mara nyingi zimekuwa zikienda na mbinu zifuatazo;

1. Nyakati za kuzuia, wapinzani wa timu hizo wamekuwa wakiaandaa mbinu za ‘kumeza’ ubora wa timu hizo kumiliki mpira kwenye sehemu kubwa ya uwanja kuzuia nyakati nyingi kwa shinikizo la chini hasa kwenye theluthi mbili za uwanja kutokea kwenye magoli yao (Mid or Low Block) ili kutoruhusu kutoa nafasi katikati au nyuma ya mistari yao ya uzuiaji itakayowafanya kutoa mwanya wa timu hizo 3 kutengeneza nafasi za kufunga magoli.

 

2. Nyakati za kushambulia, wapinzani wa timu hizo 3 wamekuwa wakitegemea mashambulizi ya kujibu au kushtukiza dhidi ya timu hizo 3 pale zinapopata umiliki wa mpira au kupora umiliki wa mpira kwa haraka kwenye nafasi zinazoachwa wazi na timu hizo kimuundo wakiwa na mpira kabla timu hizo 3 hazijarejea kwenye muundo wao bora wa kuzuia (Counter Attacks) kwani ni ngumu kuzifunga zikiwa kwenye muundo mzuri wa kuzuia.

 

Timu 3 za juu zimeiabiliana vipi na Counter Attacks?

Kwasababu timu hizo 3 'kubwa' zimekuwa wahanga wa kufanyiwa mashambulizi ya kujibu wakicheza dhidi ya timu 'ndogo', timu hizo mara nyingi zimekuwa zikitumia mbinu zifuatazo kuzuia Counter Attacks;

- Kuanza kuzuia kwa shinikizo kubwa eneo walipopotezea umiliki wa mpira (Counter Pressing)

- Wachezaji kurudi kwenye maeneo sahihi kimuundo kwa haraka (Recovery Runs)

- Kuwa na umbo rafiki kwenye mistari miwili ya nyuma kuzuia mashambulizi ya kujibu (Rest Defence/Offensive Balance)

Kwasababu sehemu muhimu kati ya hizo 3 ni umbo linaloachwa na timu kwenye mistari miwili nyuma pindi timu inapokuwa kwenye nusu ya wapinzani  'Rest Defence' leo tutaona faida za watu muhimu wanaounda umbo hilo la kumeza Counter Attacks

 

Timu hizo zote licha kutumia mifumo mama kama 4-2-3-1, 4-4-2 na 4-3-3 kama mifumo yao mama (Basic Formation) lakini zikiwa na umiliki wa mpira hasa kwenye theluthi mbili za mwishi zimekuwa zikitumia muundo wenye umbo la 2-1 kwenye mistari miwili ya nyuma inayohusisha mabeki wawili wa kati na kiungo mmoja mbele yao (Rest defense)

 

- Kwenye mechi 23 za ligi kuu ya NBC, Rest defense ya Azam FC imeundwa na Himid Mao mbele ya mabeki tofauti wa kati kama Yeison Fuentes, Yoro Diabi, Twalib Nuru na Lameck Lawi

- Kwenye mechi 27 za Ligi kuu ya NBC, Rest defense ya Simba SC imeundwa na Yussuph Kagoma na mabeki tofauti Kama Rushine De Reuck, Ismail Toure, Hussein Mbegu na Vedastus Masinde

- Kwenye mechi 29 za Ligi kuu ya NBC, Rest defense ya Young Africans imeundwa na Duke Abuya na mabeki tofauti wa kati kama Dickson Job, Ibrahim Hamad na Bakari Mwamnyeto na Frank Assink

 

Viungo hao wa kati wamekuwa mhimili mkubwa kuweza kuzuia mashambulizi ya kujibu kabla ya kufika kwa mabeki na makipa wao wakisimama mara nyingi mbele ya mabeki wao na kuwa kama bima kuwapa uhuru wachezaji wa mbele kuwa wabunifu wakijua kuwa kuna watu wanawalinda pindi wao wakipoteza mpira.

Kuthibitisha ubora huo licha ya kuwa timu hizo kushambuliwa kwa Counter attacks mara kwa mara zimekuwa timu zinazoongoza kwa kufungwa idadi ndogo ya magoli kama ifuatavyo;

 

1. Young Africans - magoli 9

2. Simba SC - magoli 11

3. Azam FC - magoli 12

 

Licha ya kutotajwa sana kwasababu hawaonekani nyakati za kufunga magoli lakini wamekuwa muhimu kwa timu zao kutofungwa magoli.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet