pmbet

UN yaishutumu Rwanda kwa kuongoza operesheni za kijeshi za M23

Eric Buyanza

July 3, 2025
Share :

Un yaishutumu rwanda kwa kuongoza operesheni za kijeshi za m23

Ripoti ya karibuni kutoka Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumatano, Julai 2, imeishutumu Rwanda kwa kuongoza 'operation' za kijeshi dhidi ya Rwanda.

Ripoti hiyo inabainisha kuwepo kwa askari wengi wa Rwanda-hadi wanajeshi 6,000-katika ardhi ya Kongo kati ya mwezi Mei 2025, na inataja majina ya maafisa kadhaa wakuu wa Rwanda waliohusika moja kwa moja katika operesheni hizo. 

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walioandika ripoti hiyo wanasema mnamo mwezi Januari na Februari 2025, takriban wanajeshi 6,000 wa Rwanda—ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa Kikosi Maalumu—walitumwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, na Rwanda iliajiri wapiganaji wa zamani wa FDLR waliorejshwa katika maisha ya kiraia kufanya shughuli za upelelezi na kijasusi katika ardhi ya Kongo.
Wakati baadhi ya wanajeshi hao walirejea Rwanda baada ya kutekwa kwa mji wa Goma, wengine walitumwa tena kuelekea mji wa Bukavu.

Pia wanabaini kwamba operesheni za Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) mashariki mwa DRC zilipangwa na kuelekezwa haswa na James Kabarebe, kamanda wa zamani wa jeshi la Rwanda ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda na aliwekewa vikwazo na Wizara ya Fedha ya Marekani mwezi Februari mwaka jana kwa kuwa na "uungaji mkono" wa Rwanda kwa AFC/M23, kulingana na Washington. Wengine waliotajwa ni Jenerali Vincent Nyakarundi, Mkuu wa Majeshi ya Rwanda na Jenerali Patrick Kauretwa, Mkuu wa Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Rwanda.

 

RFI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet