pmbet

Unaelewa nini kuhusu kupatwa kwa mwezi ?.

Joyce Shedrack

September 8, 2025
Share :

Kupatwa kwa Mwezi (kwa Kiingereza: lunar eclipse) ni badiliko la mwangaza na rangi ya Mwezi kwa muda.

Kunatokea wakati wa Mwezi kupita katika kivuli cha Dunia ambako nuru ya Jua haifiki kwenye uso wa Mwezi moja kwa moja.

When to see March 2025 total lunar eclipse, blood moon | 13newsnow.com

''Mwezi unaangazwa na nuru inayoakisiwa na Dunia na kuwa na rangi nyekundu(21. Kwa hiyo Mwezi huwa na nuru hafifu ukionekana mwekundu katika kipindi cha kupatwa.

 

Badiliko hili linatokea tu wakati wa mwezi mpevu linaweza kudumu saa moja hadi nne. Baadaye Mwezi unatoka tena katika kivuli cha Dunia unaonekana kama mwezi mpevu wa kawaida.

 

Kupatwa kwa Mwezi kunasababishwa na kivuli cha Dunia kinachomwaga giza juu ya Mwezi wote kabisa au baadhi ya sehemu.

Hali hii inatokea wakati Mwezi - Dunia na Jua vikiwa vimekaa katika mstari mmoja, ikiwa Dunia iko kati ya Jua na Mwezi. Hapo kivuli cha Dunia kinafunika Mwezi.

 

Inatokea tu wakati wa mwezi mpevu. Hali hii ni kinyume cha kupatwa kwa Jua ambako Jua, Mwezi na Dunia vinakuwa pia katika mstari lakini hapo Mwezi uko kati ya Jua na Dunia na hivyo ni Mwezi unaosababisha giza kwenye uso wa Dunia pale ambako kivuli chake kinapita juu ya Dunia.

 

SEHEMU ZILIZOLIONA TUKIO
Kwa mujilou wa TMA, tukio hili limeonekana katika mabara ya Ulaya, Asia, Australia no Afrika, ambapo nchini Tanzania hali ya kupatwa kwa mwezi limeanza kuonekana kuanzia saa 2:29 usiku. Tukio lote limekadiriwa kudumu kwa takribani sad sita.

HISTORIA YA MATUKIO YA KUPATWA KWA MWEZI KARIBUNI
lli kuonesha mwendelezo wa matukio ya aina hii, kumbukumbu za hivi karibuni ni pamoja na 26 Mei 2021 - "Super Flower Blood
Moon".
 kupatwa kamili kwa mwezi.
* 16 Mei 2022 - Kupatwa kwa mwezi kamili lililodumu zaidi ya saa moja.
* 8 Novemba 2022 - Kupatwa kwa mwezi kamili lililoshuhudiwa sehemu kubwa ya dunia.
* 14 Machi 2025 - Tukio la kupatwa kwa mwezi kamili lililotokea miezi michache

MAANA ZA KITAMADUNI NA KIIMANI
Katika tamaduni mbalimbali duniani, kupatwa kwa mwezi kumekuwa na maana tofauti:
Nchini India, tukio hilli hujulikana kama Chandra Grahan, ambapo jamii huamini ni muda wa kujitakasa na kufanya ibada
maalum.
* Katika historia ya Kiafrika, baadhi ya jamii zilihusisha kupatwa na ishard za mabadiliko ya msimu au matukio muhimu ya kijamii.

FAIDA KWA JAMII
Zaidi ya mitazamo ya kiimani na kifalsafa, kupatwa kwa mwezi ni tukio la kielimu na kijamii: 

Hutoa fursa kwa wanafunzi na walimu kujifunza somo la anga kwa njia ya moja kwa moja.
* Ni tukio linalowaunganisha watu duniani kote, bila kujali mipaka ya taifa, kwani wote hushuhudia jambo moja la
asili.
* Ni njia ya kuimarisha sayansi katika jamii, kuhimiza utafiti na hamasa ya kizazi kipya kwenye masuala ya anga.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet