pmbet

Unaijua 'Chameleon Style' ya Rulani na Mamelodi? Hizi hapa Mbinu zake

Sisti Herman

March 28, 2024
Share :

Utangulizi

 

Kwenye moja ya mahojiano yake kocha mkuu wa Mamelodi Sundowns Rulani Mokwena anabainisha kuhusiana na namna timu yake inavyocheza, akianza kwa simulizi hii;

 

"Rafiki yangu ambaye mmoja wa watathmini wa viwango wa moja ya timu kubwa Ulaya, alinipigia simu baada ya mechi, nikamuuliza na imani utakuwa umeburudika, akanijibu sikujua hata mlikua mnacheza mfumo gani, nami nikamjibu 'Naam hili ndilo nililohitaji' kutotabirika" 

 

- Rulani anasema wakati na timu yake ya ufundi wakifanya tathmini ya maandalizi ya msimu mpya misimu iliyopita waling'amua kuwa mbinu zao za uchezaji kwa misimu miwili mfululizo zimekuwa wazi sana kiasi kwamba imekuwa rahisi kwa kila wapinzani wanaoenda kukutana nao kujua kwa urahisi ubora na udhaifu wao.

 

Mbinu zao zilizokuwa wazi ni zipi?

 

Awali Rulani alitumia mbinu zenye idadi kubwa ya viungo na kutumia zaidi mifumo ya 4-3-3 na 4-4-2 diamond wakiwa na staili ya kumiliki mpira zaidi kwa kuwa na muda na nafasi kubwa kuwa na utawala wa mchezo.

 

Rulani alipenda kutumia mfumo wa 4-4-2 na 4-3-3 wakiwa wanashambulia, ambapo eneo la kiungo mara nyingi lilikiwa na viungo wanne kwenye umbo la Diamond ambapo;

 

  • Kiungo mmoja hubaki mbele ya mabeki

  • Viungo wawili hucheza kwenye nafasi kati ya wachezaji wa pembeni na wa kati wa timu pinzani (Inside channels)

  • Kiungo mmoja mshambuliaji hucheza nyuma ya viungo wa timu pinzani

 

- Kwenye muundo huu mchezaji muhimu zaidi alikua Themba Zwane ambaye alikua kama mshambuliaji kivuli, wakizuia hucheza kama mshambuliaji Sambamba na Sirino/Mailula na Shalulile na Wakishambulia hushuka katikati ya mstari wa mabeki na viungo wa timu pinzani kuwa kama kiungo mshambuliaji.

 

- Pia, wachezaji wa pembeni kwenye muundo huu walitumika kama Viungo wa pembeni kushambulia mapana ya uwanja, Aubrey Modiba na Thapelo Morena/Khuliso Mudau

 

Kwanini walibadilishana mbinu?

 

Kwenye tathmini yao anathibitisha kuwa waligundua mapungufu kadhaa ya kimbinu yaliyowalazimu kubadilishana Mbinu, kama;

 

- Njia zao za kushambulia (patterns of play) kulingana na mifumo hiyo kutabirika kirahisi na kisha wapinzani kuja mbinu nzuri za kuwazuia, mfano;

 

  • Kukaa wengi nyuma ya mpira na kuwaachia mpira watawale Possession kwenye theluthi mbili za mwanzo

  • Kuzuia njia za kati na pembeni wakati wa kupenya kuta zao na Kutengeneza nafasi kwenye theluthi ya mwisho

 

- Kushambuliwa kwa mashambulizi ya kujibu kabla hawajarejea kwenye miundo yao ya uzuiaji pindi wakipokonywa mpira (negative transitions) kumbuka Mamelodi nyakati nyingi huwa na mpira na wachezaji hutawanyika sana

 

Baada ya kung'amua hayo madhaifu wakaboresha na kuja na Mbinu alizoita "Chameleon type of approach".

 

‘Chameleon type of approach’ ya Rulani ipoje?

 

Rulani anabainisha kuwa baada ya mbinu zao za awali kutabirika, yeye na timu yake waliamua kuja na staili ya kumwendea mpinzani kulingana na ubora na udhaifu wao, kimbinu au kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, staili ambayo hubadilika kulingana na mpinzani aina ya mpinzani anayeendewa, hubadilika kama Kinyonga au "Chameleon type of approach", ambayo;

 

- Mifumo ya uchezaji hubadilika kulingana na namna wapinzani walivyo bila kuathiri misingi na staili za uchezaji kulingana na falsafa zao

- Uchaguzi wa Kikosi, muundo na namna ya uchezaji kutegemea mbinu za wapinzani

- Hubeba ubora wote wa mbinu zao za awali

- Na Kuboresha madhaifu

 

Tabia za "Chameleon type of Approach" ya Rulani

 

1. Pressure Attraction & Space Creation - Kulazimisha wapinzani watengeneze nafasi

 

- Rulani anasema waling'amua kuwa kuwa wapinzani hupenda kubaki nyuma ya mpira na kufinya uwanja kwenye theluthi zao mbili za mwanzo (Low & Mid Block) ili kumeza ubora wa mbinu zao

 

- Hivyo wakaamua kuwekeza kwenye wazo la kuwa na kipa kisasa ambaye anaweza kusaidia timu kujenga mashambulizi kuanzia kwenye theluthi ya kwanza ya ujenzi wa mashambulizi (Modern Goalkeeper) ambapo walimsajili Ronwen Williams mwanzoni mwa msimu wa 2022/23 kutokea Supersport United

 

- Faida za kuwa na kipa wa kisasa kwenye ujenzi wa mashambulizi ni pamoja na;

 

  (i) Mipira yote ya kuanzisha (Goal Kick) ambayo zamani ilikuwa ikipigwa kuanzia langoni kwa pasi ndefu za juu, tafiti ziliongesha mingi hupotea kwani ukishakuwa juu huwa wa kushindaniwa na wachezaji wa pande zote mbili, hivyo kwa uhakika wa kuwa wa upande wa timu inayoanzisha inabidi uanze kumilikiwa kuanzia kwenye theluthi ya kwanza wakijenga shambulizi

 

  (ii) Kujenga mashambulizi kwa pasi fupi kuanzia kwenye theluthi ya mwanzo (Building from back) huwatamanisha na kuwashinikiza wapinzani kuwafuata na wakiwa fuata huacha nafasi nyuma, aidha katikati ya mistari ya uzuiaji au nyuma ya mstari wa mabeki

 

- Timu inayozuia inapoanza kuwafuata Mamelodi Sundowns wanaojenga shambulizi kuanzia kwenye miguu ya Ronwen Williams, haacha nafasi nyuma kutokana mambo makuu mawili;

 

   (i) Wakizuia kuanzia mbele huku umbo lao la uzuiaji (Pressing structure) likiwa halina nidhamu nzuri nafasi ndogo Katikati ya mistari yao ya uzuiaji ina maana Mamelodi hufaidika na nafasi hizo na kuvuka kupitia njia za katikati (Passing through the press)

  (ii) Wakizuia kuanzia mbele huku umbo lao la uzuiaji likizuia kwa nidhamu kubwa ya kufinya nafasi, Mamelodi Sundowns hufanya makadirio ya kupita juu na kulenga nafasi nyuma a ya mstari wa mabeki wa timu inayozuia (Passing Over the press)

 

- Hivyo faida ya kipa wa kisasa ni uwezo wake wa kiufundi kucheza kama mchezaji wa ndani na kujenga mashambulizi kuanzia nyuma, jambo ambalo hushawishi wapinzani kuwafuata na kuacha nafasi kwenye maeneo hayo mawili

 

2. Verticality - Matumizi sahihi, fanisi na ya haraka ya mianya katikati mistari ya kina cha uzuiaji cha wapinzani baada ya kuwavuta 

 

Rulani huamini Kwenye staili ya kucheza kwa kumfuata mpinzani kwake kwakupenya na njia za katikati na sio kupitia pembeni kwenye mapana ya uwanja, na;

 

- Ili kuweza kufika kwenye lango la wapinzani lazima Uelekeo wa mashambulizi uwe kwenye lango lao 

- Pia huamini ili Uelekeo wa mashambulizi uwe kwenye lango lao lazima mistari ya muundo wa uzuiaji wa wapinzani ivunjwe kwa pasi na mikimbio

- Ili kurahisisha uvunjaji wa mistari ya uzuiaji ya wapinzani ni lazima kina chao cha uzuiaji kiwe kirefu na Kutengeneza mianya

- Ili watengeneze mianya ni lazima wafuate Build up za Mamelodi kuanzia nyuma ili kuwe na umbali mkubwa kati mstari wa mbele (washambuliaji), kati (Viungo) na wa nyuma (mabeki) ya uzuiaji ya wapinzani

- Hivyo kadiri nafasi zinavyojitengeneza pindi wanapovutika, ndiyo wachezaji wa Mamelodi hukaa kwenye maeneo Katikati ya mistari yao 

 

Mbinu za Mamelodi hupanga wachezaji kwenye miundo tofauti kulingana na nafasi Katikati ya mistari ya uzuiaji ya wapinzani na mara nyingi huwa na Muundo wa 3-2-2-1-2, ambapo;

 

- Nyuma hubaki watu watatu, dhidi ya washambuliaji wa timu pinzani

- Mbele yao Viungo wanne kwenye umbo la boxi au Diamond, ambao huwa wengi dhidi ya Viungo wa timu pinzani 

- Mbele yao huwepo Kiungo mmoja ambaye huwa huru

- Mwisho huwa na washambuliaji wawili

 

Umbo hili hutawanya wachezaji kuongeza kina cha kushambulia kuelekea kwa wapinzani na kurahisisha mashambulizi kuvunja mistari ya uzuiaji ya wapinzani kuelekea langoni kwao na sio kwenye mapana ya uwanja (Positional Superiority), Lakini pia mara kadhaa huwa kwenye muundo wenye wachezaji wa pembeni kama;

 

- 4-4-2 diamond ambayo huwa 2-4-2-2, umbo la katikati huwa boxi au Diamond huku mabeki wa pembeni wakicheza kwenye mapana ya uwanja

- Pia hutumia mchezaji wa pembeni wa upande mmoja 

 

3. Numerical Superiority - Kutengeneza idadi kubwa kila idara

 

Kwenye kila hatua ya shambulizi la Mamelodi, Rulani ametumia kupandikiza mbinu zinazowazidi wapinzani wao idadi, mfano;

 

(i) Wakiwa kwenye theluthi ya kwanza (Build up phase), hufaidika na kuongezeka kwa idadi kwa kumtumia kipa wa kisasa, Ronwen Williams kama mchezaji wa ndani, na muundo wao kutoka nyuma huwa na watu watatu ambao huzidi idadi mistari ya Kwanza ya uzuiaji ya Pressing Structure tofauti za wapinzani, mfano;

 

  • Wapinzani wanaotumia 4-2-3-1, huwa 3v1

  • Wapinzani wanaotumia 4-4-2, huwa 3v2

  • Wapinzani wanaotumia 4-3-3, huwa 3v3

 

 (ii) Wakiwa kwenye theluthi ya pili na ya mwisho ya uwanja (Middle & Final Third) hubadili miundo ili waweze kuendeleza shambulizi, kupenya kuta za uzuiaji za wapinzani kulingana na namna wapinzani wnaavyozuia njia, hasa za kati, mfano;

 

  • Kutumia mabeki wa kati wanaoingia eneo la kati (Inverted Full-backs), anaweza kuwa wa upande mmoja au wote wawili, mfano Modiba na Mudau, faida kubwa ni kuwa na idadi kubwa ya viungo wanaoweza kusaidia timu kuendeleza mashambulizi. 

 

  • Kutumia beki wa kati mmoja anayejongea usawa wa kiungo wa kati (Progressive Center Backs), mara nyingi Coetzee husogea usawa wa Mokoena kuwa Viungo wawili wa kati mbele ya mabeki watatu na kufanya kiungo wa kati mwingine, mara nyingi Allende kusogea usawa wa kiungo mshambuliaji Themba Zwane kuwa na Layer mbili za Viungo kwenye umbo la sanduku (Box Midfield), wawili wakiendeleza shambulizi kutoka kwa kipa au mabeki (Build up Progressions), wawili husaidia upenyaji na utengenezaji wa nafasi (Penetrations and Chances Creations).

 

4. Rest defence - Muundo bora kuzuia mashambulizi ya kujibu (Rest defence)

 

Mamelodi wakimiliki mpira kwenye nusu ya mpinzani muundo wao wa uchezaji hutengeneza muundo mzuri kwenye mistari miwili ya nyuma kiasi kwamba kama wapinzani watapokonya mpira na kushambuliwa kwa COUNTER ATTACKS basi muundo wa nyuma hufanya timu kuwa salama, kwasababu;

 

- Idadi ya wachezaji wengi

- Aina ya wachezaji kwenye mistari hiyo

 

Idadi ya wachezaji kwenye mistari hiyo miwili huwa wachezaji watano, mfano;

 

- Msimu wa 2022/23 walitumia Rest defence inayohitaji mabeki wa pembeni kati ya wanne kuingia eneo la kiungo (Inverted Full-backs), shape yao ikawa 2+3, Mfano Mudau, Modiba na Mokoena mbele ya Mvala na Kekana.

- Msimu wa 2023/24 walitumia Rest defence inayohitaji beki mmoja wa kati, kati ya Wanne kuingia eneo la kati usawa wa kiungo (Progressive Center Back) na Kutengeneza shape ya 3+2, Mfano Coetzee na Mokoena mbele ya Kekana, Mvala na Lebusa

 

Rulani aligundua kuwa Rest defence ya 2+3 ya msimu wa 2022/23 ina mapungufu kama kutoweza kuhimili mipira mirefu ya juu Kutokana na aina ya wachezaji aliokuwa nao ndiyo maana msimu wa 2023/24 akaja na Rest defence ya 3+4 ambayo wachezaji wa nyuma wana vimo virefu kuweza kuhimili mipira mirefu.

 

Faida ya Rest defence ni kuwa wachezaji wa mbele huwa huru kuonyesha ubunifu Kwa uhuru (Risk taking) wa kuweza kupenya na Kutengeneza nafasi wakiwa na uhakika kuwa endapo watapoteza mpira basi kuna Bima ya Rest Defence (Calculated Risk)

 

5. Versatility - Wachezaji Kuboreshwa uwezo wa kiufundi kucheza nafasi na majukumu tofauti uwanjani

 

- Moja kati ya ubora mkubwa wa Sundowns msimu huu ni namna ambavyo wanafanya Uchaguzi wa Kikosi chao, kikosi himubadilika mara kwa mara lakini timu inaendelea kuwa na kiwango kilekile

 

- Alipoulizwa huzingatia kipi kwenye upangaji wa Kikosi chale Rulani Mokwena alitaja mambo mawili;

 

(i) Meritocracy - Uchaguzi kuzingatia faida za wachezaji kulingana na mahitaji ya mbinu za kuwavaa wapinzani kulingana na ubora na udhaifu wao

(ii) Squad Management - Uchaguzi wa Kikosi kuzingatia ukomo wa nishati ili kuzuia majeraha na uchovu kwa wachezaji

 

- Mambo haya mawili yamekuwa yakifanya Kikosi cha Sundowns kubadilika mara kwa mara kulingana na Mbinu za wapinzani

- Pia kwasababu Mbinu za Sundowns hubadilika kulingana na aina ya wapinzani wanaocheza nao, Wachezaji wamekuwa pia wakibadilishiwa majukumu na ikibidi nafasi za kucheza kulingana na aina ya wapinzani wanaoenda kucheza nao, mfano;

 

(i) Aubrey Modiba ameshawahi kucheza kama beki wa pembeni, kiungo wa kati, kiungo mshambuliaji na winga

(ii) Thapelo Morena ameshawahi kucheza kama beki wa pembeni, mshambuliaji , Winga na kiungo 

(iii) Grant Kekana ameshawahi kucheza kama Beki wa kati, pembeni 

(iv) Rivaldo Coetzee hucheza kama beki wa Kati lakini pia kama kiungo wa kati

(v) Mothobi Mvala hucheza kama beki wa kati na Kiungo wa kati pia

 

Hao ni mfano tu na wengine wengi wamekuwa kama "VIRAKA" wana-fit popote penye uhitaji

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet