United yafuzu fainali 'kwa mbinde' dhidi ya timu ya daraja la 1
Sisti Herman
April 22, 2024
Share :
Klabu ya Manchester United jana imeshinda 'kwa mbinde' kwenye nusu fainali ya pili ya kombe la FA dhidi ya timu ya ligi daraja la kwanza ya Uingereza Coventry baada ya sare ya kustaajabisha ya 3-3 na kisha kufuzu kwa kushinda matuta.
Sare hiyo ya kustaajabisha ilitokana na namna Man Utd walivyofanyiwa 'Come back' baada ya kuongoza mabao matatu kisha kusawazishiwa mabao yote huku goli la ushindi la Coventry likikataliwa na mwamuzi.
Mabao ya United kwenye mchezo huo yalifungwa na Scott McTominay dakika ya 23, Harry Maguire dakika ya45 pamoja na Bruno Fernández dakika 58.
Mabao ya Coventry kwenye mchezo huo yamefungwa na Simms dakika ya 71, O’Hare dakika ya 78, Wright (p) dakika ya 95.
Baada ya sare hiyo kwenye dakika 90 za mchezo mechi hiyo ya mtoano ikamuuliwa na matuta 4-2, United wakaungana na City kwenye fainali itakayochezwa dimba la Wembley, London.