Upasuaji wa kwanza bila kufungua kifua wafanyika Tanzania
Eric Buyanza
December 15, 2023
Share :
Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete(JKCI) kwa kushirikiana na madaktari kutoka India wamefanikiwa kubadilisha valvu ya moyo bila kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa mara ya kwanza nchini.
Upasuaji huo ujulikanao kuwa wa tundu dogo ulichukua saa moja umefanywa kwa watu watatu ambao hali zao zinaendelea vizuri sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKC, Dk Richard Kisenge amesema upasuaji huo umefanywa na wataalamu wazawa kwa asilimia 90 na kueleza kuwa awali wagonjwa wenye tatizo hilo walikuwa wakipelekwa nje ya nchi.
“Upasuaji huu unafanyika Ulaya na Asia na kwa Afrika wanaofanya ni Afrika Kusini, Misri, Tunisia na Morocco na hakuna hospitali ya Serikali Afrika inayofanya aina hiyo ya upasuaji,”amesema.
Amesema upasuaji huo unagharimu kiasi cha Sh milioni 80 ndani ya nchi huku nje ya nchi ukiwa ni Sh milioni 150.