pmbet

Ureno mzigoni leo Georgia na Czech kukufua matumaini ya kusalia Ujerumani.

Joyce Shedrack

June 22, 2024
Share :

Baada ya siku ya jana Timu ya taifa ya Poland kuwa timu ya kwanza kufifisha matumaini ya kusalia kwenye michuano ya kombe la Mataifa Ulaya 2024 kufuatia sare ya Ufaransa dhidi ya Uholanzi na kusababisha kundi hilo kuongozwa na Ufaransa mwenye alama 4,Uholanzi alama 4,Austria alama 3 na Poland ambaye hajawahi kuvuna alama hata moja, leo pengine tukashuhudia timu nyingine itakayosubiri nafasi ya best looser ili kufuzu hatua inayofuata  ya michuano hiyo.

 

Siku ya leo kutapigwa michezo 3 katika mashindano hayo huku miwili ikizikutanisha timu za kundi F ambapo Uturuki atacheza na Ureno, na Georgia atakutana na Jamhuri ya Czech ili kuamua msimamo wa F.

 

Mpaka sasa msimamo wa kundi F upo hivi

Uturuki - 3

Ureno- 3

C. Republic -0

Georgia - 0 .

 

Kwenye mashindano hayo  kila kundi linatakiwa kutoa washindi wawili watakaofuzu hatua ya 16 moja kwa moja na mshindi wa tatu kwa kila kundi atakayeingia kama best looser.

 

Unadhani nani safari yake imeishia hapa kwenye michuano hii ?.

 

Mchezo mwingine utakaopigwa leo nje ya kundi hilo ni Belgium vs Romania. 

 



 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet