Ureno yafuzu kinyonge robo fainali EURO 2024
Sisti Herman
July 2, 2024
Share :
Timu ya Taifa ya Ureno jana ilifanikiwa kufuzu kwa 'Mbinde' hatua ya robo fainali ya kombe la Mataifa Ulaya (EURO 2024) baada ya kuwatoa Slovania kwa mikwaju ya penati 3-0 baada suluhu kwenye dakika 120 za mchezo huo.
Ureno ilipewa nafasi kubwa dhidi ya Slovenia ambapo dakika ya 105 walipata mkwaju wa penalti ambao ungeweza kumaliza mechi lakini nahodha na mshambuliaji wao kinara Cristiano Ronaldo akakosa baada ya juhudi za kipa wa Slovenia Jan Oblak kuokoa mkwaju huo.
Kwenye hatua ya mikwaju ya penalti, Slovenia walikosa penalti zote walizopiga huku kipa wa Ureno Diogo Costa akiibuka shujaa baada ya kuzidaka zote.
Kwa upande wa Ureno, Cristiano Ronaldo, Bruno Fernandez na Bernado Silva walifunga penalti zote 3 zilizowapa ushindi.