Ureno yatangaza Rafael Leao kuvaa jezi namba 7kwenye mechi 2 zijazo.
Joyce Shedrack
October 1, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Ureno, Rafael Leão, anatarajiwa kuvaa jezi namba 7 ya timu ya taifa katika michezo miwili ijayo baada ya namba hiyo kuachwa wazi kufuatia kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kambini siku ya jana.

Namba 7 imekuwa jezi ya historia katika timu ya taifa ya Ureno iliyovaliwa kwa miaka mingi na Ronaldo na sasa Leão amepewa nafasi ya kuivaa katika michezo hiyo miwili punde tu baada ya Ronaldo kuondoka kambini licha ya kuwa hajatangaza rasmi kustaafu kuichezea Timu ya Taifa.
Hatua hiyo imezua gumzo miongoni mwa mashabiki wa Ureno huku baadhi yao wakiweka wazi kuwa ni usaliti wa hali ya juu kwa Ronaldo ambaye amekuwa nguzo kubwa ya mafanikio ya Ureno.





