Ureno yatwaa kombe la dunia U17 2025
Sisti Herman
November 27, 2025
Share :

Ureno imeshinda taji la Kombe la Dunia la FIFA la vijana chini ya miaka 17 (U-17) 2025, kwa kuwalaza Austria 1-0 kwenye fainali iliyomalizika hivi punde.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa Benfica Anísio Cabral dakika ya 32.
Hili ni taji la kwanza la Ureno la U-17 Kombe la Dunia.
Mashindano hayo yalifanyika Qatar kuanzia Novemba 3 hadi Novemba 27, 2025.





