pmbet

Urusi inatumia 'Sumu za kuzuia pumzi' vita vya Ukraine – Marekani

Eric Buyanza

May 2, 2024
Share :

Marekani imeishutumu Urusi kwa kutumia silaha za kemikali kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine kinyume na sheria za kimataifa zinazopiga marufuku matumizi hayo.

Imesema Urusi ilitumia kemikali ya 'Chloropicrin' kupata mafanikio ya kivita dhidi ya Ukraine.

Ikulu ya Urusi hata hivyo haijatoa maoni yoyote, lakini ilikanusha vikali madai kama hayo yaliyotolewa siku za nyuma.

'Chloropicrin' ambayo Marekani inasema Urusi imetumia ilitumiwa sana wakati wa Vita vya kwanza vya Dunia.

Utumiaji wa kemikali katika vita umepigwa marufuku chini ya mkataba wa CWC.
BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet