Urusi watumia kombora la Hypersonic kuishambulia Ukraine
Eric Buyanza
May 25, 2026
Share :

Mji mkuu wa Ukraine na viunga vyake uLIshambuliwa vikali na jeshi la Urusi usiku wa Jumamosi, Mei 23, kuamkia Jumapili, Mei 24, ikiwa ni pamoja na kombora la balistiki la Oreshnik, na kuua watu wasiopungua wanne.
Saa chache mapema, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Ubalozi wa Marekani huko Kyiv walielezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa shambulio la Urusi lililokuwa likiandaliwa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin aliahidi kujibu kijeshi kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye majengo ya elimu katika eneo la Luhansk, lililotokea usiku wa Alhamisi, Mei 21, kuamkia Ijumaa, Mei 22.
Taarifa zinasema takriban milipuko kumi mikubwa ilisikika saa 7:00 usiku, kabla ya mashamblizi mengine kulikumba jiji kutoka nchi kavu, angani na Baharini.
Mamlaka imesema zaidi ya watu 60 walijeruhiwa, meya wa mji mkuu, Vitali Klitschko, ameandika kwenye Telegram. Ameongeza kuwa shule katika wilaya ya Shevchenkivsky pia ililengwa. Shambulio "karibu" na shule nyingine lilisababisha vifusi kuziba mlango wa makazi ambapo wakazi walikuwa wakikimbilia, ameongeza.
RFI





