pmbet

Urusi yadungua karibu droni 350 za Ukraine

Eric Buyanza

May 8, 2026
Share :

Urusi leo Ijumaa imesema kuwa imezindungua droni zilizorushwa kuelekea Moscow muda mfupi baada ya kuonya kuhusu uwezakano wa shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Ukraine licha ya kutangaza usitishaji mapigano wa siku mbili kwa ajili ya maadhimisho ya Vita vya Pili vya Dunia.

 

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kwamba vikosi vyake vimezindungua karibu droni 350 za Ukraine zilivurumishwa usiku kucha.

 

Saa chache kabla ya kuanza kwa usitishaji mapigano wa Urusi, Rais wa UkraineVolodymyr Zelensky aliwaonya washirika wa Urusi kutohudhuria gwaride hilo.
 

Hapo jana pia, kiongozi huyo aliikosoa Urusi kwa kupendekeza kusitisha mapigano siku ya Mei 8-9 ilihali ilipuuza pendekezo lao la kusitisha mapigano siku ya Mei 6 na badala yake Urusi iliishia kufanya mashambulizi yaliyowaua watu kadhaa.

 

DW

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet