Urusi yahusishwa na majeneza ya Ufaransa yaliyoachwa kwenye mnara
Eric Buyanza
June 4, 2024
Share :
Maafisa wa kijasusi wa Ufaransa wanaamini kuwa Urusi inahusika na majeneza matano yenye bendera ya Ufaransa na yenye maandishi "Wanajeshi wa Ufaransa wa Ukraine" yaliyowekwa karibu na Mnara wa Eiffel.
Wanaume watatu walionekana wakiwasili kwa gari eneo la tukio siku ya Jumamosi na kuacha majeneza hayo ambayo baadae yaligundulika kuwa na magunia ya plasta ndani yake.
Polisi inamshikilia raia wa Bulgaria aliyekuwa dereva wa gari hilo aliyedai amelipwa euro 40 kufikisha mzigo hapo.
Baadaye, polisi waliwakamata watu wengine wawili katika kituo cha basi katikati ya mji wa Paris, ambapo inadaiwa walikuwa wakipanga kupanda basi kuelekea Berlin.
Waliwaambia polisi walikuwa wamelipwa euro 400 kuweka majeneza hayo, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.
Kumekuwa na sintofahamu miongoni mwa mataifa hayo mawili haswa baada ya Rais wa Ufaransa kutaka kupeleka askari wake nchini UKraine na pia kutoa msaada wa silaha kwa nchi hiyo.