Urusi yaichimba mkwara Marekani, yasema itatoa jibu la kijeshi
Eric Buyanza
July 11, 2024
Share :
Urusi itatoa jibu la kijeshi kwa mipango ya Marekani ya kupeleka makombora ya masafa marefu nchini Ujerumani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Ryabkov alisema Alhamisi.
"Tutajibu jambo hili kwa utulivu, Jeshi tayari limeanza kulifanyia kazi suala hili na tutatoa jibu la kijeshi kwa tishio hili jipya" Waziri Ryabkov aliwaambia waandishi wa habari.