pmbet

Urusi yaionya Ufaransa, ukipeleka wanajeshi Ukraine unatafuta shida!

Eric Buyanza

April 5, 2024
Share :

Mawaziri wa Ulinzi wa Urusi na Ufaransa wamefanya mazungumzo ambapo Urusi imeitahadharisha Ufaransa dhidi ya mpango wake kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine.
 

Mazungumzo hayo kwa njia ya simu kati ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu na mwenzake wa Ufaransa Sebastien Lecornu ni ya kwanza baina ya viongozi hao wawili katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja na nusu.
 

Taarifa iliyotolewa na Moscow imesema Shoigu amemweleza kinagaubaga Lecornu kwamba iwapo serikali mjini Paris itatekeleza kile ilichokusudia juu ya uwezekano wa kutuma kikosi cha jeshi la Ufaransa nchini Ukraine, basi jambo hilo litasababisha matatizo kwa Ufaransa yenyewe.
 

Hata hivyo taarifa hiyo haikufafanua zaidi kuhusu maana ya tahadhari hiyo iliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu.
 

Suala hilo limeibuka kwenye mazungumzo baina ya viongozi hao wawili kufuatia matamshi ya Rais Emmanuel Macron aliyoyatoa mwezi Februari, ambapo alisema haondoi uwezekano kwa nchi za magharibi kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet