pmbet

Urusi yapambana usiku kucha, yadungua droni 660 za Ukraine

Eric Buyanza

June 26, 2026
Share :

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza leo ljumaa kuwa imefanikiwa kuzuia droni 660 za Ukraine zilizorushwa usiku kucha katika mikoa 12 ya Urusi.
 

Maeneo yalioathirika na shambulizi la Ukraine ni pamoja na eneo la Crimea lililotekwa kinyume cha sheria na pia juu ya Bahari ya Azov na Nyeusi.

 

Katika mkoa wa Tula, ulioko kusini mwa Moscow, nyumba moja iliharibiwa kutokana na shambulio hilo na mwanamke mmoja kujeruhiwa. Haya ni kulingana na taarifa iliyochapishwa mtandaoni na gavana wa eneo hilo Dmitry Milyaev.

 

Pia amesema njia ya kusambaza umeme iliharibiwa pamoja na kituo kimoja cha viwanda katika mji wa Novomoskovsk.

 

Shirika la habari la Astra, nchini Urusi, limeripoti kuwa kiwanda cha kemikali na kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji mjini Novomoskovsk vilishambuliwa na kushika moto.

 

Hata hivyo, taarifa hiyo haikuweza kuthibitishwa kwa njia rasmi na mamlaka pia haijatoa tamko rasmi.

 

Meya wa Moscow, Sergei Sobyanin, pia amesema droni 47 za Ukraine zilidunguliwa zilipokuwa zikielekea mji mkuu wa Urusi. Hakuripoti vifo wala uharibifu wowote.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet