Urusi yasema imedungua droni 8 kutoka Ukraine
Eric Buyanza
July 7, 2025
Share :
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vya ulinzi wa anga vya nchi hiyo, vimedungua droni 8 za Ukraine kati ya 90 zilizorushwa katika eneo la Crimea na bahari nyeusi.
Wizara hiyo imesema droni nyingi zilizodunguliwa zilianguka katika maeneo yaliyoko karibu na Ukraine na droni tatu ziliharibiwa katika eneo la Leningrad lililo karibu na mji wa pili kwa ukubwa nchini Urusi wa St Petersburg.
Kwa kawaida wizara ya ulinzi nchini Urusi huwa inaripoti tu kuhusu idadi ya droni zilizodunguliwa na hairipoti kuhusu hasara iliyotokea.
Hata hivyo magavana wa maeneo yaliyoshambuliwa wamesema uharibifu wa majengo haukuwa mkubwa.