Urusi yasema imekiteka kijiji cha Rozdolivka, mashariki mwa Ukraine
Eric Buyanza
June 29, 2024
Share :
Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema jana (Ijumaa jioni) kuwa imefanikiwa kukiteka kijiji cha Rozdolivka, kilichopo katika jimbo la Donetsk mashariki mwa Ukraine na wanajeshi wa Urusi wanaendelea kusonga mbele.
Wizara hiyo ilisema katika taarifa yake kwamba baada ya mapambano makali jeshi lake lilifanikiwa kuviondoa vikosi vya Ukraine kwenye kijiji hicho.