Urusi yateka kijiji cha Vovtche nchini Ukraine
Eric Buyanza
July 30, 2024
Share :
Jeshi la Urusi limedai kuwa leo Jumatatu, Julai 29, limekiteka kijiji Vovtche kilichopo katika jimbo la Ukraine la Donetsk, ambapo jeshi la nchi hiyo linaendelea kusonga mbele likiwa linapambana na vikosi vichache vya Ukraine tena visivyo silaha za kutosha.
Mapigano ni makali katika eneo la Donetsk na jeshi la Urusi linaelekea katika mji wa Pokrovsk.
Siku ya Jumapili Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema imechukua udhibiti wa vijiji vya Prohres na Yevhenivka, vyote vilivyo umbali wa kilomita 30 mashariki mwa Pokrvovsk.