Urusi yatuma droni kushambulia mjii mkuu wa Ukraine, Kyiv
Eric Buyanza
July 31, 2024
Share :
Urusi imefanya mashambulizi ya kushtukiza ya kutumia droni kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na maeneo jirani usiku wa kuamkia leo. Taarifa hizo zimetolewa na uongozi wa kijeshi wa Ukraine kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram.
Kiongozi wa kamandi ya kijeshi ya mji wa Kyiv Serhiy Popko amesema mifumo ya ulinzi wa anga ilifanya kazi ya kuzidungua droni juu ya anga la mji huo. Mashuhuda waliozungumza na shirika la habari la Reuters wamesema walisikia milio inayooaminikia kuwa ni ya makombora ya mifumo ya ulinzi wa anga yanayotumika kudungua droni au ndege za adui.
Eneo kubwa la mji huo mkuu lilikuwa chini ya hali ya tahadhari ya kutokea mashambulizi ya anga tangu saa mbili usiku jana Jumanne.