Urusi yaudhibiti mkoa wa Luhansk nchini Ukraine
Eric Buyanza
July 1, 2025
Share :
Urusi imesema imekamilisha udhibiti wa mkoa wa Luhansk ulioko mashariki mwa Ukraine.
Mkoa wa Luhansk tayari ulikuwa unadhibitiwa kwa kiasi na wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi tangu mwaka 2014, lakini vita vilivyozuka Februari 2022, vimeiwezesha Urusi kukamata sehemu kubwa ya mkoa huo.
Urusi mpaka sasa imeshaiteka mikoa ya Luhansk, Donesk, Zaporizhzhya na Kherson.