pmbet

Urusi yauteka mji wa Dnipropetrovsk nchini Ukraine

Eric Buyanza

August 27, 2025
Share :

Jeshi la Ukraine limekiri kuwa majeshi ya Urusi yamevuka na kuingia katika mkoa wa viwanda wa Dnipropetrovsk, mashariki mwa nchi hiyo, na kujaribu kujikita katika eneo hilo.

 

Afisa wa kundi la kijeshi la Dnipro, Viktor Trehubov, ameiambia BBC kuwa huu ndio mashambulizi ya kwanza ya kiwango kikubwa katika mkoa huo, ingawa alisisitiza kuwa jeshi la Ukraine limefanikiwa kusimamisha kasi ya adui.

Urusi imekuwa ikidai mara kwa mara kuwa majeshi yake yameingia Dnipropetrovsk kupitia Donetsk, ambapo mapigano makali yamekuwa yakiendelea.

 

Mwezi Juni, viongozi wa Urusi walitangaza kuanza kwa operesheni katika eneo hilo, lakini ripoti za hivi karibuni kutoka Ukraine zinaonesha kuwa wapiganaji wa Urusi wamepenya kidogo tu katika mpaka wa mkoa huo.

 

Mkoa wa Dnipropetrovsk, ambao kabla ya vita ulikuwa na wakazi zaidi ya milioni tatu, ni kituo kikubwa cha pili cha viwanda nchini Ukraine baada ya Donbas (inayojumuisha Donetsk na Luhansk).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet