USAJILI WA RODRI: Mourinho akasirishwa na uzembe wa Madrid
Eric Buyanza
August 7, 2026
Share :
Kocha wa Real Madrid, José Mourinho, amekasirishwa sana na kitendo cha Barcelona kufanikiwa kuipiku Madrid katika mbio za kumnasa kiungo wa Manchester City, Rodri.
Taarifa zinasema amefadhaishwa na namna uongozi wa Real Madrid ulivyolichukulia suala hili kwa kusuasua.
Mourinho alikuwa ameuomba uongozi wa Madrid ukamilishe usajili wa Rodri haraka iwezekanavyo baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia ya kujiunga nao. Hata hivyo, Madrid walichukua muda mrefu kujadiliana na Man City wakijaribu kushusha bei.
Wakati Madrid wakisuasua, Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Deco, na kocha Hansi Flick walifanya mazungumzo ya haraka na Rodri na kufanikiwa kumshawishi.






