"Usajili wetu safari hii unafanyika kwa umakini wa ICU"Ahmed Ally.
Joyce Shedrack
July 10, 2025
Share :
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amewatoa hofu mashabiki wa Simba kuhusu suala la usajili kwenye klabu yao katika dirisha hili kubwa la usajili huku akithibisha kuwa baadhi ya wachezaji tayari wamesajiliwa na usajili unafanyika kwa umakini mkubwa.

“Mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuna taarifa za usajili kuhusu Simba wengine wanaihusisha Simba kwenye kila mchezaji ili kuwapa thamani Wachezaji wanaotaka kuwasajili”.
“Taarifa tu ni kwamba usajili wetu safari hii unafanyika kwa umakini wa ICU, na Wachezaji waliopendekezwa na Mwalimu wameshasajiliwa na wengine wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili”
“Kwa sasa tunamalizia kutoa barua kwa wale tunaochana nao kisha tuanze kuvurumisha Thank You na baada ya hapo tuanze kudondosha chuma kimoja baada ya kingine”.Ameandika Ahmed Ally.