pmbet

Usher aandika rekodi mpya Super Bowl

Sisti Herman

February 14, 2024
Share :

Nyota wa muziki wa R&B kutoka Marekani Usher Raymond amevunja rekodi katika Tamasha la Super Bowl Half Time akiwa ndiye Msanii aliyetazamwa zaidi akiwapita wasanii wengine waliowahi kushiriki onyesho hilo miaka iliyopita kama Rihanna, Katy Perry, Beyonce, Dr. Dre, Madonna na wengineo.

 

Kwa mujibu wa takwimu za CBS News, Onyesho hilo limefikisha Watazamaji milioni zaidi ya milioni 12 na kuvunja rekodi zilizowekwa kabla kama ile ya Rihanna iliyofanyika mwaka 2023 ikiwa na Watazamaji milioni 12.

 

Usher aliungana na mastaa wengine kama Alicia Keys waliyeimba naye wimbo wa 'My Boo' na baadaye Ludacris, Lil Jon, will.i.a.m na H.E.R walipanda jukwaani kukamilisha dakika 13 za nguvu kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika wakati wa mapumziko kwenye kilele cha ligi ya mchezo wa American Football.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet