Usher kuacha pombe kisa Show
Sisti Herman
January 9, 2024
Share :
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Usher Raymond ameamua kuacha matumizi ya Pombe na vinywaji vyenye sukari kwa ajili ya kujiandaa na onesho la Super Bowl Halftime litalofanyika Allegiant nchini humo mwezi Febuari 11 mwaka huu.
Inaelezwa kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 45 ameamua kuacha vitu hivyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki katika onesho hilo alilokuwa akilisubiri kwa zaidi ya miaka kumi.
Mwanamuziki huyo amewahi kufanya nyimbo kama OMG, Good Good, ‘Hey Daddy’, ‘My Boo’, ‘Dientes’, ‘Yeah!’, ‘U got it Bad’, na nyingine nyingi.