pmbet

"Usifanye hivyo", Biden aiomba Iran isiishambulie Israel

Eric Buyanza

April 13, 2024
Share :

Rais wa Marekani Joe Biden ana wasiwasi mkubwa kuwa Iran inajipanga kuishambulia Israeli hivi karibuni.

Hata hivyo Rais huyo wa taifa kubwa duniani ameitaka Iran kutokufanya hivyo. 

"Usifanye hivyo" ni ujumbe wa Joe Biden kwa Iran kwa kifupi. 

“Sitaki kutoa taarifa za siri, lakini nina wasiwasi kuna kitu kitatokea hivi karibuni. Tumejitolea kwa ulinzi wa Israeli. Tutaiunga mkono Israel. Tutaisaidia Israel kujilinda na Iran haitafanikiwa,” rais wa Marekani amesema.

Maafisa wa Marekani wanakataa kueleza kwa undani zaidi taarifa za kijasusi walizonazo, lakini Mshauri wa Mawasiliano wa Usalama wa Kitaifa John Kirby ana uhakika na tishio hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet