‘Usiruhusu mtoto aende shule kukiwa na mvua kubwa’ - Prof Mkenda
Eric Buyanza
April 25, 2024
Share :
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewataka wazazi na walezi wasiwaruhusu watoto kwenda shule mvua ikiwa inanyesha kubwa.
Prof. Mkenda amesema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ni vyema wazazi wakachukua tahadhari kuepusha majanga.
“Mzazi ukiona mvua ni kubwa usimruhusu mtoto wako aende shule, akikosa siku moja au mbili si vibaya, tunazipongeza shule ambazo zimeshachukua hatua za kusitisha masomo kipindi hiki,” amesema.
Hatua hiyo inatokana na mvua kubwa zinazonyesha na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara kupitika kwa shida pamoja na baadhi ya shule kuzingirwa na maji.
Jumanne, Aprili 23, 2024, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitangaza mwendelezo wa mvua katika mikoa mbalimbali nchini na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.