Usitumie vijiti vya meno 'toothpick' utasababisha meno kusogea - Mtaalam
Eric Buyanza
July 22, 2024
Share :
Bingwa wa Upasuaji, Kinywa, Meno na Uso, Dk. Gemma Berege, ameisa jamii kuepuka matumizi ya vijiti vya meno (Toothpick), wanapohitaji kuondoa vipande vya chakula vilivyosalia kwenye ya meno, kuepuka kusogeza meno na kuharibu msingi wake.
“Matumizi ya ‘toothpick’ kama yalivyozoeleka kwenye jamii hatuyashauri. Vijiti hivi unapotumia mara kwa mara husababisha msingi wa meno ambao ni fizi kuharibika na meno kusogea, utaharibu taswira ya sura na mdomo.” amesema Dk. Berege.
NIPASHE