pmbet

Usyk amchapa Tyson Fury mbele ya Ronaldo na AJ

Sisti Herman

May 19, 2024
Share :

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Ukraine Oleksandr Usyk amemchaka Tyson Fury wa Uingereza kwa pointi za majaji wawili (Split Decision) na kuwa ‘Undisputed Champion’ wa kwanza tangu Lennox Lewis na wa kwanza katika historia ya uzito wa juu zama hizi za mikanda minne.

Pointi za majaji zilikuwa kama ifuatavyo jaji namba moja alitoa pointi 115-112 faida kwa Usyk, jaji namba mbili alitoa pointi 114-113 faida kwa Fury na jaji namba tatu alitoa 114-113 faida kwa Usyk.

Usyk anaichukua mikanda yake ya WBA, IBF, WBO & IBO alafu anaijumuisha na ile aliyompora Fury WBC, Ring Magazine & Lineal Heavyweight, hakika ni rekodi ya kuvutia sana.

Hili ni pambano la kwanza kwa Fury kupoteza katika mapambano 36 tangu aanze kucheza ngumi za kulipwa, huku ukiwa ni ushindi wa 22 kwa Usyk katika mapambano 22 alioyacheza kwenye ngumi za kulipwa.

Usyk anaandika rekodi ya kuwa ‘Undisputed Champion’ katika madaraja mawili ya uzito, alikuwa ‘Undisputed Champion’ wa uzito wa Cruiserweight na sasa kwenye uzito wa juu.

Tangu Novemba mwaka 1999 dunia haikushuhudia pambano la ubingwa wa Undisputed katika uzito wa juu, hadi baada ya miaka 25 usiku wa kuamkia leo historia ikiandikwa mjini Riyadh, Saudi Arabia.

 

Pambano hilo la kihistoria pia liihudhuriwa na mastaa wakubwa kama Cristiano Ronaldo na Antony Joshua

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet