Utafiti: 70% ya Gen Z hawapati usingizi
Sisti Herman
February 19, 2026
Share :

Utafiti mpya unaonyesha kuwa silimia 70 ya vijana wa Gen Z wanatatizika kulala usiku kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa kifedha, kupanda kwa gharama za maisha pamoja na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi.
Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Marekani ya Amerisleep unaonyesha katika hilo vijana wengi huripoti kuhisi kulemewa na upangaji bajeti, kuweka akiba.
Vijana wengi wanasema daima wana wasiwasi kuhusu jinsi ya kusimamia bajeti yao, kulipa kodi ya nyumba, na kuendelea na gharama za kila siku, juu ya wasiwasi kuhusu utulivu wa kazi na siku zijazo.
Badala ya kupumzika, wao hukaa kwenye simu zao au kwenye televisheni, wakijaribu kujizuia kutoka kwenye shinikizo, lakini wanashindwa.





