pmbet

Utafiti: Idea nyingi huja wakati wa ukiwa bafuni au chooni

Sisti Herman

April 14, 2026
Share :

 

Kwa mujibu wa Zac Irving, Profesa msaidizi wa Falsafa na mtafiti wa Chuo kikuu cha Virginia ameeleza kuwa mawazo mengi ya kibunifu huja wakati mtu akiwa bafuni wakati wa kuoga au chooni wakati wa haja.

Mwanafalsafa huyo ameeleza kuwa Kitaalamu kitendo hicho kinaitwa "The Incubation Effect" au "The Shower Effect."

Unapokuwa unajikita kufikiria tatizo gumu kwa nguvu (Focused Mode), akili inakuwa kwenye mkazo (stress).

Unapoacha kufikiria jambo hilo na kufanya kitu kingine cha kawaida, kama kuoga, kutembea, au kufanya usafi - akili inaingia kwenye hali inayoitwa "Diffuse Mode."

Katika hali hiyo haya ndio baadhi ya mambo ambayo hutokea:

- Subconscious Processing: Ingawa wewe unaona kama umepumzika, akili yako ya ndani (subconscious) huwa inaendelea kufanya kazi "chini kwa chini." Inachukua vipande vya habari ulivyokuwa navyo awali na kuanza kuvipanga upya kwa namna ambayo hukuweza kufanya ulipokuwa umekaza ubongo.

- Dopamine Release: Shughuli kama kuoga huufanya mwili kutoa homoni ya dopamine, ambayo hupunguza msongo wa mawazo na kuifanya akili kuwa huru zaidi. Hali hii inaruhusu mawazo ya kibunifu (creative insights) kutiririka kirahisi.

- Kupumzika kwa "Prefrontal Cortex": Hii ni sehemu ya mbele ya ubongo inayohusika na maamuzi na mantiki. Unapooga, sehemu hii inapumzika kidogo, hivyo inaruhusu sehemu nyingine za ubongo kuanza "kuongea" zenyewe, jambo linalozalisha yale mawazo mapya ya ghafla.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet