pmbet

Utafiti; Tanzania nchi ya 3 Afrika Wafanyakazi wake kuwa na 'Stress'

Sisti Herman

June 5, 2024
Share :

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya tatu kwenye orodha ya nchi ambazo wafanyakazi wengi hufanya kazi wakiwa na kiwango cha juu cha msongo wa mawazo.

Ripoti ya kampuni ya utafiti ya Gallup ya Hali ya Wafanyakazi Duniani 2023 inaripoti na kuwakilisha sauti ya wafanyakazi, ikichunguza kiwango cha msongo wa mawazo kwa watu wanaofanya kazi Afrika na ripoti imegundua kuwa kuna ongezeko la wafanyakazi wanaofanikiwa kazini, hata wakati msongo wa mawazo wa wafanyakazi ukiendelea kuwa kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hii ni orodha ya nchi 10 zenye wafanyakazi wenye msongo mkubwa wa mawazo;

1. Chad - 58%
2. Uganda - 57%
3. Tanzania - 56%
4. Tunisia - 56%
5. Ghana - 54 %
6. Sierra Lione - 53%
7. Senegal - 50%
8. Nigeria - 50%
9. Guinea - 49%
10. Libya - 49%

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet