Utafiti: Wanawake huvutiwa na wanaume wenye vitambi
Sisti Herman
March 31, 2026
Share :

Utafiti mpya uliotolewa kwenye jarida la kisayansi Personality and Individual Differences umebaini kuwa, kwa wastani, wanawake wengi huonesha mvuto mkubwa zaidi kwa wanaume wenye tumbo kubwa (higher waist-to-hip ratio) kuliko wale waliokonda kupita kiasi.
Kwa mujibu wa watafiti, katika baadhi ya mazingira hasa yale ambayo kihistoria yalikuwa na uhaba wa chakula umbo la mwili lenye kitambi linaweza kuhusishwa bila kujitambua na afya, uthabiti pamoja na upatikanaji wa rasilimali.
Hali hiyo inaweza kuwa moja ya sababu zinazochangia namna mvuto wa kimapenzi unavyoundwa, ambapo si kila wakati mwili mwembamba ndio unaoonekana kuvutia zaidi.
Hata hivyo, wataalamu wanasisitiza kuwa mvuto wa kimapenzi hutofautiana kulingana na mtu, tamaduni na mazingira, hivyo matokeo hayo hayawezi kutumika kwa kila mtu.





