Utafiti wasitishwa baada ya mtoto wao kuanza kuwa na tabia za sokwe
Eric Buyanza
March 1, 2024
Share :
Mwaka 1931 wanasayansi wawili Luella na Winthrop Kellog (mke wa mume) walikuwa wanafanya utafiti ambapo walimchukua sokwe mtoto aliyekuwa na umri wa miezi saba na kujaribu kumlea pamoja na mtoto wao wa kiume aliyeitwa Donald aliyekuwa na umri wa miezi 10 wakati huo, dhumuni la utafiti wao ilikuwa ni kutaka kuona kama yule mtoto sokwe atajifunza tabia za kibinadamu
Wanasayansi hao walianza kumlea mtoto wao pamoja na yule sokwe kama 'kaka na dada', ambapo utafiiti ulienda kwa miezi 9 huku wakichunguza vitu vingi ikiwemo tabia zao na namna wanavyowasiliana na kucheza.
Hata hivyo iliwabidi wasitishe utafiti wao haraka baada ya kuja kugundua kuwa mtoto wao Donald alianza kuishi na kuwa na tabia kama za sokwe.