pmbet

Utafiti; Zanzibar ni kisiwa cha pili kinachovutia zaidi duniani 2024

Sisti Herman

May 11, 2024
Share :

Utafiti mpya uliofanywa na Bounce umeitaja Zanzibar kuwa sehemu ya pili ya visiwa vinavyovutia zaidi duniani kwa mwaka 2024, na kuyashinda maeneo mengine yenye hadhi ya juu kama vile Mallorca, Ibiza na Sardinia.

Utafiti huo umezingatia mambo kadhaa kama mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo kwa Zanzibar halijoto hukadiriwa kuwa nyuzijoto 28°C na mvua ya hadi milimita 401

Lakini pia gharama nafuu za utalii ambapo ikilinganishwa na maeneo mengine, bei za hoteli Zanzibar hubakia chini kwa wastani wa $160 kwa usiku, hata hivyo visiwa kama vile Bali, Indonesia, huamuru bei ya wastani ya $1,870 kwa usiku.

Visiwa 10 bora kwenye Orodha ya utafiti;

1. Phuket, Thailand
2. Zanzibar, Tanzania
3. Krete, Ugiriki
4. Puerto Rico, Karibea
5. Mallorca, Uhispania
6. Cozumel, Meksiko
7. Mauritius
8. Aruba
9. Bali, Indonesia
10. Ibiza, Uhispania

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet