pmbet

Utafutaji wa mahari unachangia wizi wa mifugo - Murkomen

Eric Buyanza

March 27, 2026
Share :

Wimbi la ujangili na wizi wa mifugo huko nchini Kenya lililosababisha vifo vya watu wengi na kuibwa kwa maelfu ya mifugo linachochewa na shinikizo za kitamaduni kwa vijana wanaotaka kuoa.
 

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Bw Kipchumba Murkomen, alisema visa vya wizi wa mifugo ambavyo vimekuwa vikikumba kaunti za Meru, Laikipia, Isiolo, Marsabit na Samburu kwa miaka mingi, vinatekelezwa na vijana wanaohitaji ng’ombe kwa ajili ya mahari.

 

Waziri huyo alizungumza Jumatatu akiwa Mbataru eneo la Tigania Mashariki, ambapo aliwahakikishia viongozi kuwa serikali imejitolea kukomesha uhalifu huo.

 

Ziara hiyo imejiri baada ya ongezeko la visa vya wizi wa mifugo ambavyo vimesababisha vifo vya watu 11 na kuibwa kwa zaidi ya ng’ombe 600 katika miezi miwili iliyopita.

 

Source: TaifaLeo

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet